• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

Watumishi 3 Manispaa ya Songea Wasimamishwa Kazi

Imewekwa kuanzia tarehe: February 17th, 2019

 

RC MNDEME-AWASIMAMISHA KAZI WATUMISHI 3 MANISPAA YA SONGEA KWA KUSABABISHA  HASARA YA TSH.118 MILIONI

Songea,                                                                                                           15.01.2019

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa watumishi watatu wa idara ya fedha  wa halmashauri ya Manispaa ya Songea

Mndeme ametoa agizo hilo leo Ijumaa wakati alipohutubia kikao cha Baraza la Madiwani maalum kwa ajili ya kupitisha bajeti ya mwaka 2019/2020 ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea.

Amemtaja mtumishi  Mhasibu (Cashier) Juliana Rocky Likunguwala kwa kosa la kusababisha hasara ya shilingi milioni mia moja na kumi na nane ambazo imebainika alizichukua kwa njia ya kutoa risiti bandia za wateja.

 Mkuu huyo wa mkoa amesema mhasibu huyo  kwa kipindi cha miezi mitano tangu Julai 2018 hadi Novemba 2018 ameibia Manispaa ya Songea kiasi cha shilingi milioni 118  za Manispaa ya Songea.

 “Mtumishi huyu Juliana Rocky anatuhumiwa kutoa risiti bandia kwa wateja wanaoleta fedha za makusanyo ya mapato ya ndani ili ziingizwe kwenye mfumo wa malipo ya serikali” amesema mkuu wa mkoa.

Mndeme amesema uchunguzi uliofanyika ulibaini kuwa mhasibu huyo alishindwa kupeleka fedha benki kwa mujibu wa utaratibu 

“Fedha hizi zilizoibwa zingeweza kujenga zahanati na hata madarasa kusaidia maendeleo ya wananchi ,lakini zimeibwa na mtumishi wa umma kinyume cha utaratibu” Mndeme amesema serikali haitosita kuchukua hatua kali kwa watumishi wanaojihusisha na ubadhirifu.

Aidha anatuhumiwa kwa kosa la kuchukua fedha za serikali na kutumia kwenye masuala binasfi kinyume na taratibu na sheria za fedha za umma

Kufuatia agizo hilo ,mkuu wa mkoa alimwagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma SACP Gemin Mushy kumtafuta na kumkamata mhasibu huyO mara moja na kutiwa mahabusu.

“RPC  mtafute Juliana popote alipo na umweke ndani masaa 48 akisubiri utaratibu wa kisheria wa kumfikisha mahakamani kutokana na ubadhirifu wa fedha za umma” aliagiza Mndeme.

Wakati huo huo Mkuu wa mkoa wa Ruvuma ameagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea  Tina Sekambo kuwasimamisha kazi watumishi wawili wa Idara ya Fedha.

Amewata watumishi hao kuwa ni Mtunza Hazina wa Manispaa ya Songea Denis Mwaitete kwa kosa la kushindwa kusimamamia idara ya fedha hata kupelekea ubadhirifu wa fedha Tsh 118 milioni

Mtumishi mwingine aliyetajwa kusimamishwa kazi ni Mhasibu wa Mapato wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea  Salum Mwaru  kwa kosa la kushindwa kusimamia vema makusanyo ya fedha za mapato ya ndani .

Mkuu wa mkoa Mndeme amechukua uamuzi wa kuwasimamisha kazi watumishi hao kufuatia uchunguzi uliofanywa na timu ya mkoa kuhusu mwenendo wa ukusanyaji mapato ya ndani katika Halmashauri za mkoa wa Ruvuma kutofanya vizuri mwaka 2018/2019

Mwisho.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.