• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WATUMISHI wa Afya Kalembo waishukuru serikali kwa nyumba bora

Imewekwa kuanzia tarehe: February 10th, 2023

WATUMISHI wa kituo cha Afya Kalembo Halmashauri ya Mji Mbinga,wameishukuru serikali kwa kuwajengea nyumba bora za kuishi  na kueleza kwamba zimewaongezea morali ya kazi na kutoa huduma bora kwa wananchi wanaofika kupata matibabu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti watumishi hao wamesema,nyumba hizo zimewafanya kuipenda kazi yao kwa sababu zimewaondolea msongo wa mawazo na changamoto ya mahali pa kuishi,tofauti na awali walipokuwa wamepanga nyumba mitaani ambazo hazikuwa na sifa ya kuishi mtumishi wa umma.

John Mtinda amesema,kutokana na mazingira ya ardhi la eneo hilo kuwa na tope jingi hasa nyakati za masika, ilikuwa vigumu kwao kufika kwa wakati inapotokea dharura ya kuhitajika kazini kuhudumia wagonjwa baada ya muda wa wakati  kutokana na ubovu wa barabara kutoka kwenye makazi yao hadi kazini.

Amesema, kujengwa kwa nyumba hizo ni faraja kubwa kwao kwani zimesaidia sana kupata mahali pazuri na uhakika pa kuishi na kuhaidi kuzitunza nyumba hizo na kuongeza morali ya utendaji wa majukumu yao ya kila siku.

Ameipongeza serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Halmashauri ya Mji Mbinga,kujenga nyumba hizo karibu na eneo la kazi na kueleza kuwa,zimemaliza kabisa changamoto ya mahali pa kuishi kwa watumishi wa kituo hicho.

Mariam William mtaalam wa maabara amesema, kabla ya nyumba hizo walikuwa wanateseka kuhudumia wagonjwa hasa nyakati za usiku kutokana na kuishi mbali na eneo la kazi,lakini sasa wanapata muda wa kutosha na wanafika kwa wakati hata inapotokea dharura ya kuhitajika kazini.

Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Mbinga Maximo Magehema amesema,mpango wa Halmashauri ya Mji Mbinga ni kuhakikisha kila kinapojengwa kituo cha afya kunakuwa na nyumba ili kuwawezesha watumishi kuishi jirani na eneo la kazi ili waweze kutoa huduma kwa wakati.

Amesema,mpango huo ni endelevu  kwa sababu utasaidia watumishi wa afya wanaoletwa na kufanya kazi katika Halmashauri ya mji Mbinga kuwa na mazingira mazuri,kuipenda  kazi yao na kutojutia kuwepo katika Halmashauri hiyo.

Amewataka wananchi,kuendelea kutumia zahanati,vituo vya afya na Hospitali zilizopo na zinazoendelea kujengwa kwenda kupata huduma za matibabu kwa sababu serikali inajenga miradi hiyo kwa lengo la kusogeza na kuboresha huduma  kwa wananchi.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.