Watumishi wa Afya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea (HOMSO wameshauriwa kujenga mahusiano mazuri baina yao na wagonjwa wakati wote wanapotoa huduma ya matibabu.
Wito huo umetolewa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea Dr. Magafu Majura wakati anazungumza katika kikao cha robo ya pili kilichowakutanisha watumishi wote kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali ya uboreshaji huduma kwa wateja kilichofanyika kwenye ukumbi wa hospitali hiyo mjini Songea.
Dr.Majura amesema kufanya kazi kwa weledi pamoja na kusimamia taratibu na sheria katika utoaji wa huduma kwa wagonjwa kunasaidia kutekeleza vyema majukumu yao.
Amesisitiza kujenga mahusiano mazuri kazini Kutailetea sifa nzuri Taasisi hiyo.
Amewataka watumishi kuwa na matumizi bora ya lugha wakati wa kuhudumia wagonjwa pamoja na kuzingatia lugha ya staha kwa wagonjwa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.