Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amewaomba wazee wa kimila kusimamia maadili kwa vijana na familia zao.
Ameyasema hayo, wakati akizungumza katika kikao cha wa wazee wa kimila na Machifu wa Mkoa wa Ruvuma kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
Amesema vijana wengi wamekosa hofu ya Mungu kutokana na baadhi ya viongozi kushindwa kuwajibika katika kutoa maadili mema kwa vijana hali liyosababisha baadhi ya vijana kuvaa mavazi yasiyofaa kwa utamaduni wa Tanzania.
“Sisi wenyewe kama wazazi tutimize wajibu wetu wenyewe wa malezi kwa Watoto wetu,tuache kulalamika”, amesema Kanali Thomas.
Kanali Thomas amemeawaahidi wazee hao kuwa atashughulikia changamoto zote wanazokutana nazo wazee zikiwemo ukosefu wa matibabu, ulinzi na kufikisha katika Mamlaka zinazohusika kuhusu ombi lao la wazee wote kupewa pensheni.
Katika kikao hicho Kanali Thomas amewataka matajiri wanao watumikisha watoto katika kazi zao za shambani waache mara moja kwa kuwa kuwatumika Watoto ni kinyume cha sheria zinazomlinda mtoto.
Kwa upande wake Mwenyekiti Msaidizi Baraza la Wazee Wilaya ya Songea Chrostoms Makukula ameiomba Serikali itoe elimu kwa wazee na kwamba amependekeza wazee wawe na wawakilishi kwenye vyombo vya maamuzi kama ilivyo kwa wenye ulemavu na wanawake bungeni.
Kwa upande wake Mjumbe Mwakilishi wa Wazee Wanawake Wilaya ya Songea Maria Luoga amewaomba wazee wenzake kukaa na vijana wao ili kuwafundisha maadili mema.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.