Hii ni picha ya kufunga mwaka 2023 katikati ni Mbunge wa Jimbo la Songea mjini ambaye pia ni Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Damas Ndumbaro akiwa na wanafunzi wake aliyowafundisha somo la Hisabati katika sekondari moja huko Hanga wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma ambao wameajiriwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Songea
Mwalimu na wanafunzi wake wamekutana kwenye hafla ya makabidhiano gari jipya lililotolewa na serikali kupitia Wizara ya Afya kwa ajili ya hospitali hiyo ambapo Dkt Ndumbaro alikuwa mgeni rasmi
Picha ya pamoja kwenye hafla ya makabidhiano gari jipya kwa ajili ya shughuli shirikishi na uratibu wa afya ambalo limetolewa na serikali kupitia Wizara ya Afya kwa ajili ya hospitali ya Rufaa ya Mkoa ,Songea.
Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo alikuwa ni Mbunge wa Jimbo la Songea mjini Dkt Damas Ndumbaro pichani katikati,wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas mrefu mwenye suti nyeusi,wa kwanza kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Ruvuma Kelvin challe ,kutoka kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Lous Chomboko na Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Ndugu Stephen Ndaki
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.