• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WAZIRI Mhagama aagiza kujengwa stendi ya kisasa Peramiho

Imewekwa kuanzia tarehe: September 18th, 2023

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama amezitaka Idara zinazohusika na ujenzi katika Halmashauri kuhakikisha zinajenga stendi ya mabasi  yenye ubora unaoendana na thamani ya fedha zilizotolewa ili kujenga Stendi  hiyo  katika Kijiji cha Lundusi, Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.

Mhe. Jenista ametoa maagizo hayo wakati akizindua mradi wa ujenzi wa Stendi ya kisasa ya magari katika kijiji hicho unaotekelezwa na Ofisi ya Rais kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) utakaogharimu  shilingi Milioni 482 ukitarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi sita tangu kuanza kwa mradi.

Amesema  katika awamu  ya kipindi cha pili cha utekelezaji, TASAF imejikita  katika masuala ya kuwezesha Kaya kutumia fursa za kukuza Uchumi na kuongeza kipato kwa kaya zenye walengwa pamoja na kuboresha upatikanaji wa huduma za Afya, Elimu na Maji Safi na Salama pamoja na miundo mbinu  ya kukuza uchumi ngazi ya jamii.

“Wananchi wanasubiri Stendi bora ya kisasa na siyo stendi mbovu,idara zinazohusika na ujenzi kwenye Halmashauri sasa kumekucha na hatutarajii eneo la manunuzi ya ujenzi yakawa ni kichaka cha upotevu wa fedha kutoka Ofisi ya Rais kupitia Mfuko wa TASAF hivyo matumizi sahihi ya fedha yajidhihirishwe katika mradi huu,” Amesema Mhe. Jenista.

Aidha  Mhe. Jenista  ametoa wito kwa wataalam kutekeleza  majukumu yao kama inavyotakiwa hasa maafisa wa Idara ya Ujenzi, Manunuzi na Fedha ili kuepuka kusuasua kwa mradi huo pamoja na kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji katika ngazi zote kuanzia hatua ya awali hadi hatua ya mwisho ya ukamilishaji wa mradi.

 “TASAF ni chombo cha Serikali ambacho kinasaidiana na vyombo vingine kusaidia jitihada za kuondoa kero ya umaskini, upatikanaji wa maji safi na salama, elimu na afya ili kujenga Jamii iliyo bora, ambayo sisi sote ni mashahidi. TASAF imeleta mafanikio makubwa katika Nchi yetu kama ilivyoainishwa katika Mpango wa pili wa Taifa wa Maendeleo wa 2020/2025 kwa kutumia dhana ya ushirikishwaji wa Jamii,”Amebainisha Waziri huyo.

Akitoa  taarifa ya  Shughuli za TASAF katika Halmashauri ya  Wilaya ya  Songea  Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi. Neema Maghembe amesema kukamilika kwa ujenzi wa Stendi hiyo ya mabasi utarahisisha usafiri kwa wananchi watakaofika katika Halmashauri hiyo kupata huduma.

“Faida nyingine ni Mazingira bora kwa wafanyabiashara eneo la stendi, kuimarisha ulinzi na usalama katika eneo la stendi kwa wasafiri na wafanyabiashara , kuongezeka kwa pato la Halmashauri , kuongeza fursa  ya ajira kwa vijana  na wananchi pamoja na huduma ya usafiri kwa wanaosafiri kutoka nje na ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea,” Ameeleza Mkurugenzi huyo.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Bw.  Shedrack Mziray ameeleza kuwa Mfuko huo umekuwa ukitekeleza miradi ya maendeleo nchini kwa lengo la kukwamua Kaya masikini na hatimaye waweze kubuni na kuanzisha miradi yao binafsi ili kumudu gharama za maisha.

“Tunafanya utekelezaji katika maeneo manne Kitaifa tunafanya Uhawilishaji  wa fedha ambapo mpaka sasa tumehawilisha  shilingi Bilioni 919.6 tangu kuanza kwa  Awamu ya kipindi cha Pili mwaka 2020  na kufikia kaya zaidi ya Milioni 1.3. Pia tumefanya miradi ya ajira za muda karibu miradi 14,236 yenye thamani ya Bilioni 169 na kutoa ajira kwa Kaya zaidi ya 660,000 pamoja na miradi ya kukuza uchumi wa kaya,” Amesema  Bw. Mziray.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.