Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho amewashauri wananchi kulifanya zao la Mahindi kuwa zao la biashara kwa siku za usoni ili kuwaletea faida zaidi.
Waziri Mhagama ametoa kauli hiyo hivi karibuni wakati anafanya Mikutano miwili ya hadhara katika vijiji vya Kikunja na Mpingi vilivyopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma
Waziri Mhagama amesisitiza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu ameendelea kutoa ruzuku ya mbolea, ambapo amesema kazi kubwa imebaki kwa wakulima kuongeza juhudi katika kilimo na uzalishaji wa mahindi na mazao mengine.
“Mwaka huu Mhe. Rais, ametutafutia masoko Nje ya Nchi, lengo letu ni kuhakikisha siku za karibuni tunafanya zao la mahindi kuwa zao la biashara ili liweze kusaidia wananchi kukuza uchumi na pato la familia.”,alisema Mhagama.
Hata hivyo amewaomba wananchi kuendelea kuweka akiba ya chakula cha familia badala ya kuuza chakula chote ili familia na nchi kwa ujumla iendelee kuwa na akiba ya chakula.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.