Waziri wa Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amepongeza mwekezaji wa Shamba la Silver Ndolela kwa uzalishaji mbegu za kilimo
Profesa Mkumbo ametoa pongezi hizo wakati alipofanya ziara ya kutembelea shamba hilo ambalo yenye ukubwa wa Hekta 5000 lililopo Halmashauri ya Madaba Mkoani Ruvuma
Amesema kuwepo kwa shamba la uzalishaji mbegu za mazao ya Mahindi, Maharage, Ngano na Viazi itasaidia kupunguza tatizo lambegu nchini na kuzidi kuwaimalishia wakulima kilimo cha uhakika na cha manufaa
“Ni muhimu sana uwekezaji huu kwa sababu moja ya changamoto ya kilimo nchini kuwepo kwa mbegu hafifu ambazo wakulima wetu wanatumia muda mrefu au inabidi walime eneo kubwa kupata mazao sasa kuwepo kwa shamba hili itasahidia sana kuboresha kilomo hapa nchini” amesema Waziri Mkumbo
Pia amesema Serikali itashirikiana nao katika kuwaboreshea upatikanaji wa miundombinu ili kuwezesha shughuli zote ziweze kufanyika kwa wakati kwani uwezekezaji uo unamanufaa kwa Serikali pamoja na Wananchi kwani upelekea kupata ajira ya moja kwa moja na zamuda.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.