• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WAZIRI MKUU awafunda watumishi wa umma Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: January 9th, 2023

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakuu wa wilaya na waganga wakuu wa mikoa yote nchini wasimamie maadili kwa watumishi wa sekta ya afya ili fedha zinazotolewa kwenye sekta hiyo ziendane na ubora wa huduma zinazotolewa kwa watanzania.

Amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuhakikisha anatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya afya, ununuzi wa dawa na vifaa tiba, hivyo dhamira yake hiyo ni lazima iendane na ubora wa huduma zinazotolewa wa watumishi katika sekta ya afya.

 Ameyasema hayo leo Jumapili (Januari 8, 2023) wakati akizungumza na viongozi wa Serikali wa mkoa wa Ruvuma, kwenye ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Songea.

 Pia, amewaagiza wakuu wa wilaya wasimamie upatikanaji wa dawa kutoka Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na Busket Fund kwani Mheshimiwa Rais Dkt. Samia anatoa fedha za ununuzi wa dawa “Hatutaki kusikia malalamiko, Serikali kila mwezi inaleta fedha za ununuzi wa dawa, wakuu wa wilaya simamieni hili.”

 Katika Hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka Wakuu wa wilaya kwa kushirikiana na Wakurugenzi na Maafisa Elimu wasimamie dhamira ya Mheshimiwa Rais. Dkt. Samia ya kutoa elimu bila malipo kaunzia darasa la awali hadi kidato cha sita kwa kutembelea katika shule na kukagua fomu za kujiunga na shule na kujiridhisha hakuna michango ya hovyo.

 Aidha, ameagiza kuwepo na usimamizi wa shughuli za ustawi wa jamii ikiwemo masuala ya kiuchumi na kwa wafanyabiashara wadogo, wakati na wa kubwa. “Ni lazima tusimamie mwenendo wa uchumi kwenye jamii zetu, shughuli ambazo zinawaingizia kipato wananchi lazima tuzisimamie na kuziimarisha, lazima tufanye tathimini kama tunafanya vizuri au la, na lazima tujikite kwenye maeneo yote ikiwemo

vijijini.”

 

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amesema viongozi katika halmashauri zote nchini ni lazima waweke utaratibu na tujikita katika kuondoa kero za wananchi pamoja na kuwa na dhana ya ushirikishwaji kwa kuwaeleza kila kinachofanyika Serikalini kwa kutumia vyombo vya habari na kufanya mikutano. “Lazima tufahamu kero zao na kusimamia kuzitatua.”

 Akizungumza kuhusu makusanyo kwenye Halmashauri nchini Waziri Mkuu ameagiza kufanyike utambuzi wa vyanzo vyote vya mapato na kiasi cha fedha kinachoingiza na kuwataka wenyeviti wa halmashairi zote nchini na Mameya kuliwekea nguvu eneo la makusanyo.

 Pia ameelekeza kuwa fedha zote zinazokusanywa katika vyanzo vyote ni lazima zipelekwe benki kabla ya kuingizwa kwenye matumizi. “Ni muhimu pia kukagua matumizi ya vyombo vyetu ya ukusanyaji wa mapato, fanyeni tathmini za mara kwa mara ya mwenendo wa makusanyo.”

 Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Festo Dugange amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia analeta fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa huduma za jamii na miradi ya maendeleo katika halmshauri hivyo viongozi katika maeneo hayo wanapaswa kusimamia fedha hizo. “Tunapaswa kusimamia na ni wajibu wetu kufanya hivyo ili tulete matunda yaliyokusudiwa na dhamira ya Rais kwa  Watanzania iweze kufikiwa”


Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.