WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajia kuanza ziara ya kikazi mkoani Ruvuma kuanzia leo Jumamosi Januari 2 hadi sita mwaka 2021.Kulingana na ratiba iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Waziri Mkuu anaanza ziara yake Januari 2,2021 katika wilaya ya Tunduru ambapo pamoja na mambo mengine Waziri Mkuu atakagua ukarabati wa shule ya Sekondari Tunduru.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo,Waziri Mkuu ataendelea na ziara yake Januari 4 kwa kutembelea Wilaya ya Mbinga ambako anatarajia kufungua jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Mbinga Mji na kuwasalimia wananchi,kisha atakagua nyumba nane za watumishi wa Halmashauri ya Mji Mbinga.
Kulingana na ratiba ya Ziara hiyo Waziri Mkuu siku ya Januari 4 ataendelea na ziara yake kwa kukagua ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami ya Mbinga hadi Mbambabay yenye urefu wa kilometa 66 kisha kuwasalimia wananchi wa Mbambabay.Kwa mujibu wa ziara hiyo siku ya Januari 5,Waziri Mkuu atatembelea bandari ya Mji wa Mbambabay ambako atakagua meli mpya ya abiria ya MV Mbeya II .Waziri Mkuu anatarajia kukamilisha ziara yake mkoani Ruvuma Januari 6 mwaka huu ambako ataondoka kuelekea mkoani Lindi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.