WAZIRI Mkuu Mstaafu mtoto wa mkulima Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda amewataka Viongozi na wataalamu kufanya mkakati wa kuanzisha soko la pamoja la uuzaji wa bidhaa ya batiki zinazotengenezwa na wajasiriamali.
Ameyasema hayo wakati alipotembelea banda la maonesho ya Nane nane la Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma lililopo katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya ambapo amesisitiza uwepo wa soko la pamoja litawawezesha wajasirimali kuwa soko la uhakika la bidhaa zao na kwamba wanunuzi watawafikia kwa urahisi
Maonesho ya kimataifa ya nanenane Kanda ya Nyanda za Juu kusini yalizinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango na yanatarajia kufungwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan Agosti nane jijini Mbeya
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.