WAZIRI wa Habari, Sanaa,Utamaduni na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe hivi karibuni amefanya ziara ya kikazi mkoani Ruvuma na kuzungumza na wadau wa Habari katika ukumbi wa Mipango uliopo ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Songea.
Katika ziara yake Waziri Mwakyembe ametembelea maeneo ya kihistoria yakiwemo Makumbusho ya Taifa ya Majimaji kutembelea mitambo ya TBC Kanda ya ziwa Nyasa,vituo viwili vya redio binafsi vya Jogoo na Key FM na hatimaye kuzungumza na wadau wa habari.
Akizungumza na wadau wa habari,Waziri Mwakyembe amesema kwa muda mrefu wanahabari hapa nchini wamedharauliwa na kukosa haki zao za msingi wanazostahili kupata kama wanahabari.
“Mimi ni mwanahabari mwenzenu, nimekulia humo potelea mbali anayeficha kidonda haponi,Hii tasinia inawezesha nchi na Demokrasia kufanya kazi,imekuwa ni kimbilio la mtu anayefeli duniani,uandishi wa habari siyo wa kupokea makapi’’,amesisitiza Mwakyembe.
Waziri wa Habari ameongeza kuwa Mwandishi ni mwalimu,ni mkalimani,ni mfasili na mchambuzi wa masuala mbalimbali na kwamba mtu yeyote ambaye hakidhi vigezo siyo mwandishi wa habari.
Hata hivyo amekiri kuwa hapo awali makosa yalifanyika kwa kuichukulia fani ya uandishi wa habari ni kama makapi ya wanaofeli ambapo mwaka 2016 iliundwa sheria na kwamba katiba inatambua uandishi wa habari ni taaluma,na kazi ya uandishi wa habari ni hatari na inampasa mwanahabari kuwekewa Bima,pia aingizwe kwenye mifuko ya hifadhi ya mifuko ya Taifa.
“Sheria ya habari imeundwa baraza Huru la Habari tulejee kwenye Misimamo tumeunda kamati ya Baraza itakuwa na mamlaka kama mahakama tumegundua bila serikali kuingiza pesa kwenye mifuko yao wengi watashindwa kusoma na kilele chake mwaka 2021 wanahabari tutakao anza nao kazi 2022 watakuwa wana elimu kuanzia Diploma na Degree’’,alisema.
“Siyo kwamba sina huruma, nina huruma sana,kuna watu wana uzoefu mkubwa lakini hawana Elimu inayotakiwa vijana wote wadogo hakikisheni mnakimbia kwenda kusoma”,alisisitiza Waziri wa Habari.
Katika hatua nyingine Waziri Mwakyembe amekoshwa shule ya Ruhuwiko Sekondari iliyopo Songea Mjini kwa kufanya vizuri katika michezo ya UMISETA kitaifa iliyofanyika mwaka 2019 mkoani Mtwara.
Kaimu Afisa Michezo Mkoa wa Ruvuma Anzawe Chaula amesema mafanikio waliyopata Kuimarisha Michezo kwa Shule za Msingi na Sekondari ngazi ya mkoa, ambapo katika mashidano ya UMISETA taifa mwaka 2019 timu ya mpira wa miguu ya mkoa wa Ruvuma iliibuka kinara kitaifa na kuchangia golikipa bora ambaye aliweza kwenda kushiriki mashindano ya Afrika Mashariki yaliyofanyika nchini Kenya.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Ufundi TBC Mhandisi Upendo Mbele amesema usikivu wa TBC Taifa KATIKA Mkoa wa Ruvuma kwa sasa ni mzuri tukilinganisha na miaka ya 80 ambapo mitambo yake ilichakaa na usikivu ulikuwa ni hafifu.
Amesema Serikali kupitia shirika lake la utangazaji ilimeamua kuweka mitambo mingine mipya ya FM ambapo hadi sasa katika nchi nzima kuna mitambo 67.
Imeandikwa na Aneti Ndonde
Ofisi ya Habari Mkoa wa Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.