Pichani wa kwanza kushoto mwenye mkasi ni Mbunge wa Songea mjini Dkt Damas Ndumbaro baada ya kukata utepe kwenye hafla ya kukabidhi gari jipya lililotolewa na serikali kupitia Wizara ya Afya kwa ajili ya hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea.
Dkt Ndumbaro alikuwa ni mgeni rasmi kwenye hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas pichani wa kwanza kulia mwenye suti nyeusi na Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Ndugu Stephen Ndaki
Baadhi ya watumishi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma wakiwa kwenye hafla ya makabidhiano ya gari jipya kwa ajili ya shughuli shirikishi na uratibu wa afya ndani ya Mkoa.Mgeni rasmi kwenye hafla ya makabidhiano ya gari hilo lililotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Afya alikuwa ni Mbunge wa Songea mjini Dkt Damas Ndumbaro.Hafla hiyo iliyofanyika kwenye viwanja vya hospitali ya Mkoa mjini Songea pia imehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.