Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe anafanya ziara ya siku mbili katika Mkoa wa Ruvuma kuanzia Agosti 12 hadi 13 mwaka huu.
Katika kutekeleza jukumu la kuhifadhi na kuendeleza historia ya ukombozi wa Afrika iliyopo Tanzania,Mheshimiwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Agosti 12 mwaka huu atafanya ziara ya kikazi ya kutembelea maeneo ya kihistoria yaliyotumika wakati wa harakati za ukombozi wa Afrika katika Mkoa wa Ruvuma. husuani katika Makumbusho ya Taifa ya Majimaji yaliyopo Mahenge mjini Songea.
Lengo la ziara hii ni kutembelea maeneo ya kihistoria na kujionea hali halisi ya uhifadhi wa maeneo hayo na kuhimiza viongozi na wananchi wa maeneo husika kutunza,kulinda na kuhifadhi vielelezo vya kihistoria ya ukombozi wa Afrika vinavyopatikana nchini.
Pia Waziri Mwakyembe Agosti 13 mwaka huu atatembelea atakagua mitambo ya Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Kanda ya Ziwa Nyasa iliyopo mjini Songea na kufanya ziara kwenye vituo binafsi viwili vya redio ambavyo ni Key FM Redio na Jogoo FM Redio vilivyopo mjini Songea.Kulingana na ziara hiyo Waziri Mwakyembe atahitimisha ziara yake kwa kuzungumza na wadau wa habari mkoani Ruvuma .
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma
Agosti 11,2020
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.