WAZIRI wa Maliasili na Utalii Damasi Ndumbaro amewaagiza wananchi wa kijiji cha Mbangamawe Halmashauri ya Madaba mkoani Ruvuma kuweka matumizi sahihi yanayoendana na uhifadhi wa Maliasili na Nyama pori.
Akizungumza katika mkutano wa Hadhara na wananchi hao amewaeleza faida za Maliasili na wanyama pori ikiwemo ujenzi wa Barabara , Shule ,Vituo vya afya na Ajira watu zaidi ya milioni 1 nchi nzima pamoja na kuleta fedha za kigeni dola bilioni 2.6.
“Usholoba ni mapito ya wanyama pori ,wanyama hao siyo wajinga wana hakili na wanakumbukumbu ndiomana Tembo akipita sehemu hata kama miaka 50 iliyopita atapita tena kwa sababu wanaishi kwenye familia na hakuna mtu anayeweza kuzaa na ndugu yake na tembo wapo hivyo ,akitaka kuzaa anakwenda kwenye familia nyingine ndiomana wanapita kwenye hizi sholoba iliakazae watoto wazuri ni sababu za kisayansi”.
Hata hivyo amesema vijiji vitakuwepo na vitaendelea kuwepo na lazima wananchi watambue vimeanzisha kwenye usholoba na kinachotakiwa ni kuangalia kwenye mpango wa matumizi ya ardhi na siyo kuwaonea wananchi.
“Njia za wanyama ni sawa na Mto huwezi kuzuia yakija nmafuriko huwezi kuzuia watakuja Tembo hapa mamia kwa mamia waue watu kwa faida ya Nani? Juzi tumesikia Jimbo la Tunduru Kusini kesi imekuwa ni Tembo kuua watu kwasababu kijiji kimeanzishwa kwenye usholoba na ni njia ya asili ya wanyama ilikuwepo na vijiji vimekuja na kukuta Usholoba upo”.
Waziri amewashukia wenyeviti wa vijiji na watendaji kuanzisha vijiji kwenye sholoba za wanyama ni kosa la viongozi hao kwasababu wanajua na baada ya kutatua tatizo wamekuwa wachochezi na kuwagombanisha wananchi na serikali yao.
Amesema Serikari ya Tanzania inawajali sana wananchi ndio maana imeleta maendeleo nakuleta umeme mpaka vijijini, na hawana mpango wa kubomoa nyumba ya mwananchini yeyote ilanikuweka matumizi sahihi ya ardhi na kuruhusu shughuli zinazoendana sambamba na uhifadhi ikiwemo kupanda miti na kufuga nyuki na ameahidi kuwaletea mizinga ya nyuki.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeti Mgema amesema kabla ya kutokea mgogoro huo walifanya mikutano ya kuwashirikisha wananchi hao ikiwemo uhifadhi wa Maliasili na wanyamapori unamanufaa mbalimbali ikiwemo mvua.
“Mimi niliwahi kufika hapa tulikaa masaa matatu na uongozi tukizungumzia habari la usholoba kila mtu alikuwa anazungumza lake wengine walidai hawajui usholoba, nilipanga kufanya mkutano na kukubaliana wapi usholoba uanzie ili wananchi wasiendelee kufanya shughuli za kibinadamu kwenye eneno hilo na niliwapa kazi hiyo watu wa Maliasili na wanyama pori”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa habari Halmashauri ya Madaba
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.