WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhemishiwa Seleman Jafo anatarajia kuanza ziara ya kikazi mkoan i Ruvuma kuanzia Desemba 16 mwaka huu.Kulingana na ratiba ya ziara hiyo iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Jafo anaanza ziara katika wilaya ya Tundurui ambapo Desemba 16 atakagua ukarabati wa shule ya sekondari Tunduru na mchana ataanza safari ya kuelekea wilaya ya Namtumbo ambako atakagua Kituo cha Afya Mtakanini.
Kwa mujibu wa ratoiba ya ziara hiyo,Waziri Jafo siku ya Desemba 17 atakuwa katika Manispaa ya Songea ambako anatarajia kukagua ujenzi wa barabara za Manispaa ya Songea,ukagua ujenzi wa Machinjio ya kisasa katika Kata ya Tanga na kuhitimisha kukagua kituo kikuu cha mabasi cha Mkoa wa Ruvuma kilichojengwa Kata ya Tanga Manispaa ya Songea.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.