Katika viwanja vya Makumbusho Mkoani Ruvuma, historia iliandikwa tena wakati Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mheshimiwa Peres Magiri, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mheshimiwa Kanali Ahmed Abbas Ahmed, alipoongoza uzinduzi rasmi wa maadhimisho ya miaka kumi na tano ya mashujaa.
Maadhimisho haya yamekuwa kiashiria muhimu cha heshima na utambuzi kwa mashujaa waliopambana dhidi ya ukoloni wa Kijerumani mnamo mwaka 1906.
Kwa mara ya kwanza, maadhimisho haya yalizinduliwa rasmi mwaka 2010, kwa lengo la kuwaenzi mashujaa hao waliopigania uhuru wa nchi.
Historia ya mapambano hayo ni yenye uchungu na uzalendo, ambapo mashujaa 67 walinyongwa na kuzikwa katika kaburi moja, huku Chifu Nduna Songea Mbano akizikwa peke yake, ikiwa ni ishara ya heshima na hofu ambayo wakoloni walikuwa nayo dhidi ya uongozi wake thabiti.
Katika hotuba yake, Mheshimiwa Magiri alieleza kuwa familia za mashujaa hao zinaiomba serikali ifanye juhudi za kurejesha baadhi ya viungo vya wapendwa wao vilivyochukuliwa na wakoloni wa Kijerumani.
Alisema kuwa kurejeshwa kwa viungo hivyo ni hatua muhimu katika kuhakikisha historia ya mashujaa hao inahifadhiwa na kuthaminiwa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Mwalimu Siwetu, Mkuu wa Shule ya Msingi Bombambili na Mwenyekiti wa Shule za Msingi Mkoa wa Ruvuma, alisisitiza umuhimu wa maadhimisho haya kwa kizazi cha sas ni kuwaelimisha vijana kuhusu historia ya mababu zao na namna walivyojitolea kupinga ukoloni.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.