Wilaya ya Nyasa, ambayo ipo katika Mkoa wa Ruvuma, imeendelea kupata maendeleo katika sekta mbalimbali.
Wilaya hii inazungukwa na Ziwa Nyasa inategemea sana uvuvi, kilimo, na utalii kutokana na mandhari yake nzuri na rasilimali za maji.
Tayari maendeleo kadhaa yamepatikana katika Uboreshaji wa barabara zinazounganisha vijiji na miji ya jirani ili kuwezesha usafirishaji wa mazao na huduma za kijamii.
Mradi wa upanuzi wa bandari za Ndumbi na sasa uboreshaji bandari ya Mbambabay na maboresho ya usafiri wa majini kupitia Ziwa Nyasa.
Ujenzi wa shule mpya ,hospitali ya Wilaya na vituo vya afya vijijini ili kuboresha upatikanaji wa huduma za msingi.
Wilaya ya Nyasa imeendelea kuvutia watalii kutokana na Ziwa Nyasa, visiwa vidogo, na mandhari ya kuvutia. Serikali imeweka mkazo katika kutangaza vivutio vya utalii wa mazingira na kitamaduni.
Pichani kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Mheshimiwa Sterwat Nombo na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Khalid Khalif
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.