• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WILAYA ya Tunduru ilivyodhamiria kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu

Imewekwa kuanzia tarehe: June 7th, 2023

JAMII imetakiwa kuwa mstari wa mbele kushirikiana na serikali katika kampeni za kuwaibua watu walio ambukizwa ugonjwa wa kifua kikuu ili waweze kuanzishiwa matibabu badala ya kuwaficha majumbani.

Wito huo umetolewa na mratibu wa kitengo cha kifua kikuu na ukoma Hospitali ya wilaya Tunduru Dkt Mkasange Kihongole, wakati wa kampeni ya uelimishaji,uibuaji na uchunguzi wa ugonjwa wa Tb iliyofanyika katika kijiji cha Chikomo Chinunje kata ya Mbesa wilayani humo.

Dkt Kihongole alisema, licha ya juhudi kubwa zinazofanywa na serikali katika kutokomeza ugonjwa huo,hata hivyo changamoto kubwa ni ushiriki mdogo wa jamii katika kutokomeza ugonjwa huo unaoendelea kupoteza maisha ya watu wengi hapa nchini.

Alisema,ugonjwa huo bado ni tatizo kubwa katika wilaya ya Tunduru kutokana na muingiliano na baadhi ya nchi jirani,kwa hiyo zinahitajika nguvu za pamoja kati ya Serikali,viongozi wa kisiasa na jamii nzima.

Alisema ili kutokomeza kabisa ugonjwa huo wilayani Tunduru,umoja na ushirikiano ni nyenzo muhimu katika kufikia malengo ya kutokomeza ugonjwa huo ifikapo mwaka 2033 ambapo amewapongeza wadau Shirika la Amref Healt Africa na MDH kwa kushiriki katika kampeni za kupambana na TB wilayani humo.

Alisema,ugonjwa wa kifua kikuu unatibika kwa mgonjwa kuwahi Hospitali na kupata tiba sahihi na kuwataka wananchi kuachana potofu kwamba ugonjwa huo hauna dawa.

Alisema,wamelazimika kurudi kwa ajili ya kufanya kampeni kwa mara ya pili katika vijiji hivyo kwa sababu hali ya maambukizi ya kifua kikuu bado ni tishio  kutokana na umbali hadi kufika katika vituo vya kutolea huduma za matibabu zinazopatikana Hospitali ya Mbesa na Hospitali ya wilaya Tunduru mjini.

Amewaomba wananchi,kutoa ushirikiano kwa  wahudumu wa afya ngazi ya jamii waliopo katika maeneo yao wanaofanya kazi ya kukusanya makohozi na kupeleka Hospitali kwa ajili ya uchunguzi.

Said Mohamed mkazi wa kijiji cha Chikomo,ameiomba Serikali kupitia wizara ya afya kuendelea kufanya kampeni za kuwaibua wagonjwa wa kifua kikuu ili  kuwasaidia walioambukizwa na ugonjwa huo waweze kupata matibabu.

Alisema,katika kijiji hicho kuna watu wanaugua Tb,lakini bado hawajapa matibabu kutokana na umbali uliopo hadi kufika kwenye vituo vya huduma na  wako majumbani,lakini kama wangepatiwa tiba sahihi wangeweza kupona na kupata nafasi ya kushiriki shughuli  mbalimbali za maendeleo.

Mwenyekiti wa kijiji cha Chinunje Bakari Chakupewa,ameipongeza Hospitali ya wilaya Tunduru kuendelea na kampeni hizo kwani zimesaidia sana kuokoa maisha ya watu wengi hasa wanaoishi maeneo ya vijijini.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.