• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

ZAO la Mkonge linavyoongoza kwa Soko Duniani

Imewekwa kuanzia tarehe: January 27th, 2022

MAAFISA ugani wa Mkoa wa Ruvuma wamepewa mafunzo juu ya kanuni bora za kilimo cha Mkonge .

Mafuzo hayo yametolewa na wataalamu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania [TARI] Tanga katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa Ruvuma.

Mkuu wa mafunzo kutoka Taasisi ya Utafiti ya Kilimo Tanzania Frank Mabagala ameeleza umuhimu wa  Mkonge  kwa sasa kutokana na mabadiliko makubwa ya tabia ya nchi.

 Amesema wakulima wamekua wakikosa mavuno kwa sababu hii TARI kwa kushirikiana na Bodi ya Mkonge Tanzania imeazimia kuhamasisha kilimo cha  Mkonge kwa wakulima wadogo katika maeneo mbalimbali Tanzania ili zao litumike kwa kuwaleta tija kwa wananchi wa Tanzania.

Mtafiti Dietram Mkapa ameeleza umuhimu wa kilimo cha zao la Mkonge halina msimu maalumu wa kupanda na linapokuwa tayari kuvunwa kwa mwaka mara mbili ,hivyo ni zao ambalo linaweza kumpatia mkulima kipato cha uhakika katika kipindi chote cha mwaka.

Mkapa amesema Mkonge ni zao linalostahimili magonjwa na halidhuriwi kirahisi na magugu na majanga mengine kama moto,Pia ameongeza kuwa pembejeo kama mbolea,viuagugu na viuatilifu katika mazingira ya kawaida sio lazima kutumika ingawa matumizi yake yanaongeza uzalishaji wa mavuno ya mapema

Amesema zao la Mkonge linaweza kuchanganywa na mazao mengine kama kunde,maharage,mahindi,alizeti,njegere na karanga.

Mtafiti ameeleza matumizi ya Mkonge kuwa unaweza kutumika katika tasnia ya kilimo,nishati,ujenzi,famasia,magari,meli,majumbani,ofisini na mazingira mengine.

Mkapa amesema   zao la Mkonge soko lake ni la uhakika hupatikana nje ya Nchi na ndani ya Nchi mmea wa Mkonge unaweza kuishi kwa kipindi cha miaka 10-25,hivyo kumuhakikishia mkulima kipato cha uhakika na kwa muda mrefu.

”Tubadili kilimo cha Mkonge kutoka uzio kuwa shamba la mkulima mdogo wa Mkonge, Halmahauri itumie zao la Mkonge kama zao mbadala katika maeneo makame na maeneo mengine yaliotelekezwa Pamoja na kutoa mafunzo kwa wakulima juu ya singa na ubora wa singa ,Halmashauri kwa kushirikiana na Bodi ianzishe vitalu mbegu bora za Mkonge katika maeneo makame”. amesema Mkapa.

 Mkonge ni moja kati ya  zao la biashara Tanzania,asili ya zao hili ni Mexico na baadae likasambaa katika nchi za India na Tanzania mwaka 1892, zao la Mkonge liliingizwa Nchini na mtaalamu wa kijerumani Dr.Richard Hindorff Ambaye alikua mtafiti wa mimea na udongo,Kutokana na mabadiliko ya hali ya uchumi nchini Tanzania serikali ya Tanzania ilipitisha sheria ya sekta ya mkonge ,1997;ambayo iliruhusu ubinafsishaji wa viwanda vinavyomilikiwa na serikali na kuanzisha Bodi ya Mkonge Tanzania.  

Imeandaliwa na Bahati Nyoni

Kutoka Ofisi ya Habari ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Januari 27, 2022.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.