Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amehitimisha Ziara yake ya Kikazi Mkoa wa Ruvuma kwa kuhutubia Maelfu ya Wananchi waliofurika Uwanja wa Majimaji Songea kwenye Mkutano wa hadhara wa kuagana na Wananchi wa Mkoa huo.
Rais Dk. Samia amesema Ziara yake mkoani humo iliyoanza Septemba 23, 2024 imekuwa na mafanikio Makubwa ambapo alitembelea Wilaya zote za Mkoa huo na kujionea namna fedha alizoleta zinatumika kutatua kero za Wananchi.
Aidha Rais Samia amewaahidi Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kuwa Serikali itaendelea kuleta fedha za kutekeleza Miradi ya Maendeleo ikiwa ni pamoja na kusimama kikamilifu Miradi inayoendelea Sasa ikamilike kwa wakati.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.