WAZIRI MKUU KUANZA ZIARA YA KIKAZI RUVUMA KESHO
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa anatarajia kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Ruvuma Kesho Oktoba 18,2023.
Taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban iliyotolewa kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa ziara hiyo inaanza Oktoba 18 na kukamilika Oktoba 19 mwaka huu.
Kanali Thomas amesema Mheshimiwa Waziri Mkuu akiwa mkoani Ruvuma atatembelea Halmashauri za Wilaya ya Namtumbo na Madaba ambapo atakagua miradi ya maendeleo,kuzungumza na wananchi na watumishi kwenye maeneo ya miradi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.