• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

ZIWA Nyasa limesheheni aina 400 za samaki wa mapambo

Imewekwa kuanzia tarehe: August 7th, 2023

 UTAFITI umebaini kuwa katika ziwa Nyasa kuna aina 400 za samaki wa mapambo
Muongoza watalii kutoka Wilaya ya Nyasa Joseph Ndomondo akizungumza katika banda la Halmashauri ya Nyasa kwenye maonesho ya kimataifa ya Nanenane jijini Mbeya ambako katika banda hilo kuna maonesho ya samaki wa mapambo kutoka ziwa Nyasa,amesema utafiti umebaini ndani ya ziwa Nyasa kuna aina 400 za samaki wa mapambo.
 Hata hivyo amesema dadi kubwa ya samaki wa mapambo wanapatikana kwenye visiwa vya Lundo,Mbambabay na jiwe la Pomonda Wilayani Nyasa

Kulingana na utafiti huo Ziwa Nyasa lina aina zaidi ya 400 za samaki wa mapambo ambao hawapatikani katika maziwa, mito na bahari sehemu nyingine yeyote katika sayari ya Dunia.

Tafiti zinaonesha kuwa katika Sayari inayoitwa Dunia,hakuna ziwa lenye samaki wa mapambo aina zaidi ya 400,ni ziwa Nyasa pekee,ambalo pia linaongoza duniani kwa kuwa na viumbe wengi katika maziwa yenye maji baridi pia ziwa hilo linaongoza kwa kuwa na maji maangavu.

Kulingana na utafiti ambao ulifanywa na Jumuiya ya nchi zilizo Kusini mwa Afrika(SADC) kwa kushirikiana na  nchi ya Uingereza kwenye ziwa Nyasa kati ya mwaka 1991 hadi 1994 na mwaka 1996 hadi 2000,ulionesha kuwa ziwa hilo lina kiasi cha tani 165,000 za samaki na kati ya kiasi hicho tani 35,000 za samaki.Ziwa Nyasa lina aina 1500 za samaki.

Ziwa Nyasa limezungukwa na nchi tatu ambazo ni Tanzania,Malawi na MsumbIji.Ziwa hilo lipo kwenye usawa wa meta 500 toka usawa wa bahari ambapo kina cha ziwa hilo ni karibu meta 750,urefu wake ni karibu  kilometa 1000 , upana mkubwa ni kilometa 80 na upana mdogo ni kilometa 15.

Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa nchini ambayo imejaliwa kuwa na maeneo ya hifadhi na vivutio vizuri vya utalii kama vile Makumbusho ya Taifa ya Majimaji, Mapango ya Chandamali,majengo ya kihistoria Peramiho, samaki wa mapambo, fukwe na visiwa katika ziwa Nyasa.

Vivutio vingine ni maeneo ya wapigania uhuru nchi za kusini mwa Afrika,mapori ya wanyamapori ya Liparamba, Selous, Litumbandyosi na misitu ya asili ukiwemo msitu katika milima ya Matogoro ambao ni chanzo cha Mto Ruvuma unaomwaga maji yake Bahari ya Hindi.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.