Mkoa wa Ruvuma umeingia mikataba 13 na wakandarasi yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni sita kwa ajili ya kutekeleza kazi mbalimbali za matengenezo ya barabara na ujenzi wa madaraja na makaravati.Mgeni rasmi katika hafla ya kuingia mikataba hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas.Meneja wa TARURA Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Wahabu Nyamzungu amesema mikataba hiyo ni utekelezaji wa hatua ya pili kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini TARURA Mkoa wa Ruvuma una mtandao wa kilometa 7146.22 ya mtandao mzima.
Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa amekubali kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan hadi sasa imetoa zaidi ya shilingi bilioni mbili kutekeleza mradi huo.Waziri Mkuu alikuwa mkoani Ruvuma katika ziara ya siku mbili ya kikazi ambayo ameifanya katika Halmashauri za Namtumbo na Madaba.
SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imetoa shilingi bilioni 3.12 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa vyumba vya madarasa 156 katika shule 68 za sekondari mkoani Ruvuma.
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.