Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ametoa rai kwa wananchi kuacha kuangaika na taarifa za corona kutoka kwenye mitandao badala yake watumie wataalam wa afya kupata taarifa sahihi za corona
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ameendelea kuwasisitiza wananchi kuvaa barakoa kwenye maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu na kutumia vipukusa mikono ili kukabiliana na ugonjwa hatari wa UVIKO 19 ambao umeingia nchini.
RC Ibuge ametoa rai hiyo wakati anazungumza na wananchi wa kijiji cha Mgazini wilayani Songea ambapo ulifanyika uzinduzi wa soko la mahindi Kanda ua Songea ambapo ametoa rai wananchi kujitokeza kuchanja chanjo ya corona ambayo inaendelea kutolewa katika Wilaya na Halmashauri zote mkoani Ruvuma.
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.