Mkuu wa mkoa wa Ruvuma christina Mndeme amesema chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Kinafungua matawi katika maeneo ya Madaba,Tunduru na Nyasa mkoani Ruvuma na kwamba serikali imepeleka maombi ya kufungua tawi la Chuo kikuu cha Mzumbe mjini Songea.Mndeme pia amesema serikali itakifungulia chuo kikuu cha AJUCO wakati wowote kikitimiza vigezo.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ametangaza ziara ya Makamu wa Rais mkoani Ruvuma ambayo inatarajia kuanza Septemba 14 hadi 17 mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amemaliza mgogoro wa wadau wa madini ya makaa ya mawe Mbinga uliokuwa unaikabili kampuni ya Market Insight Limited Coal hali iliyosababisha Kampuni hiyo kusitisha shughuli za uchimbaji katika kata ya Ruanda wilaya ya Mbinga tangu Desemba 2019.
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.