MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ametoa rai kwa wadau wa watalii kuvitangaza vivutio vilivyopo ukanda wa kusini ili kufungua milango ya uwekezaji.Ametoa rai hiyo wakati anafunga tamasha la Majimaji Selebuka ambalo limefanyika kwa siku nane kwenye uwanja wa michezo wa Majimaji mjini Songea.Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Zainabu Telaki akizungumza kwenye tamasha hilo ametoa rai kwa wadau wa utalii kuhakikisha kuwa vivutio vyote vilivyopo kwenye mikoa mitatu ya kusini vinatangazwa kwenye luninga zote zilizopo nchini ili kufungua fursa za utalii kusini.
Naibu Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Husein Bashe amesema serikali kupitia NFRA inatarajia kuanza kununua mahindi kwa bei ya shilingi 500 kwa kilo kuanzia Agosti Mosi mwaka huu.
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.