Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema idadi ya wanaume wanaojitokeza kupima virusi vya UKIMWI Kwenye vituo vya kupimia inaongezeka kila siku na kusababisha idadi ya wanaume kuwazidi wanawake.Alikuwa anazungumza na kikundi cha watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI cha JIPE moyo kilichopo katika kijiji cha Uyahudini kata ya Litapwasi wilaya ya Songea.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesikitishwa na kitendo kilichofanyika na wananchi wa Matemanga wilaya ya Tunduru kuharibu miundombinu ya maji ya bomba na kuacha maji yanapotea bure huku serikali ikitumia gharama kubwa kujenga miundombinu hiyo ambayo inatakiwa kulindwa na kutunzwa.
Mkuu wa Mkoa Ruvuma Christina Mndeme amekagua mradi wa maji wa Mkongogulioni wilaya ya Namtumbo ambao umetekelezwa na Serikali kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni mbili.Mradi unatarajia kuhudumia watu zaidi ya 8000.Wananchi hao hawajawahi kupata maji ya bomba tangu mwaka 1961.
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.