Eneo la Tulila lililopo katika maporomoko ya Mto Ruvuma mpakani mwa wilaya za Songea na Mbinga ni kivutio cha uwekezaji na utalii.
Rais Samia Suluhu Hassan amepangua wakuu wa mikoa na kuteua wapya akiwemo David Kafulila, Amos Makalla na Queen Sendiga ambaye aligombea urais katika uchaguzi mkuu mwaka 2020 kwa tiketi ya chama cha ADC.Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Mei 15, 2021 na mkurugenzi wa mawasiliano ya rais Ikulu, Gerson Msigwa inaeleza kuwa wateule hao wataapishwa Ikulu, Dar es Salaam Mei 18, 2021.Kafulila kada wa zamani wa NCCR-Mageuzi na Chadema ameteuliwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Arusha kuchukua nafasi ya Idd Kimanta aliyestaafu.Kafulila aliyeanzisha safari yake ya siasa katika vyama vya upinzani, aliwahi kuwa mbunge wa Kigoma Kusini na baadaye kuteuliwa kuwa katibu tawala wa Mkoa wa Songwe ambako mwaka 2020 aliachia nafasi hiyo na kujitosa kuwania ubunge Kigoma Kusini kwa tiketi ya CCM lakini alianguka katika kura za maoni.Katika uteuzi huo, Makalla ambaye amewahi kuwa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ameteuliwa tena kuwa mkuu wa mkoa huo kuchukua nafasi ya Aboubakar Kunenge aliyehamishiwa Pwani kuchukua nafasi ya Evarist Ndikilo ambaye amestaafu.Queen ameteuliwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Iringa kuchukua nafasi ya Ali Hapi aliyehamishiwa Tabora huku Rosemary Senyamule akiteuliwa kuuongoza Mkoa wa Geita akichukua nafasi ya Robert Gabriel aliyehamishiwa Mara kuendelea na wadhifa huo.
Serikali imetoa shilingi milioni 500 kuboresha Kituo cha afya Kalembo wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.Kituo hicho kilifunguliwa mwaka 2003 na Aliyekuwa Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ally Shein.
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.