Halmashauri ya Wilaya ya Songea kwa kushirikiana na AGATEO HOPE FOUNDATION inatekeleza mradi wa urasimishaji wa viwanja na mashamba lengo likiwa ni kuhakikisha kila kipande cha ardhi kinapimwa na kuwanufaisha wananchi na serikali.
Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma ACP Simon Marwa Maiga amewatahadharisha wagombea katika uchaguzi mkuu wanapofika katika mkoa huo kueleza Ilani zao kwa wananchi na kujiepusha na lugha za matusi
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma christina Mndeme amesema chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Kinafungua matawi katika maeneo ya Madaba,Tunduru na Nyasa mkoani Ruvuma na kwamba serikali imepeleka maombi ya kufungua tawi la Chuo kikuu cha Mzumbe mjini Songea.Mndeme pia amesema serikali itakifungulia chuo kikuu cha AJUCO wakati wowote kikitimiza vigezo.
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.