Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ameagiza kuchukuliwa hatua kwa wote walihusika na ubadhirifu wa ujenzi, mradi wa hospitali ya Halmashauri ya Madaba na kwamba ametoa siku 60 mradi huo kukamilika kwa asilimia 100.Serikali imetoa shilingi bilioni 1.8 kutekeleza mradi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa kwa kupata hati safi na kuwawezesha wanawake,vijana na watu wenye ulemavu mikopo kwa asilimia 100.RC Ibuge ametoa pongezi hizo wakati an azungumza kwenye kikao maalum cha Baraza la madiwani la Halmashauri hiyo cha kujadili taarifa ya CAG inayoishia Juni 30 mwaka 2021.Kikao hicho kilifanyika mjini Mbambabay kwenye ukumbi wa Kapteni Komba.
Halmashauri ya Mji wa Mbinga mkoani Ruvuma imeongoza katika ukusanyaji mapato ya ndani kwa kuweza kukusanya kwa asilimia 109.Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akizungumza kwenye kikao cha Baraza maalum la madiwani wa Halmashauri hiyo kilichofanyika kwenye ukumbi wa Odo Mwisho mjini Mbinga cha kujadili taarifa ya CAG inayoishia Juni 30,2021,ameipongeza Halmashauri hiyo kuibuka kidedea na kwamba Halmashauri ya Mbinga Mji pia kwa miaka mitano mfululizo imeweza kupata hati safi kufuatia taarifa ya ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2020/2021.
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.