Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amewaomba viongozi wa Umoja wa makanisa mkoani Ruvuma kufanya maombi maalum ya kuondoa pepo la kuvuta na kulima bangi ili kupunguza madhara makubwa yanayowapata wanaovuta bangi
Mtaalamu Mwandamizi kutoka Mamlaka ya usimamizi wanyamapori Tanzania (TAWA) akiwa na timu ya wataalam amefanya ziara ya kikazi kukagua kisiwa cha Lundo ziwa Nyasa ambapo amesema kisiwa hicho kinafaa kwa Wanyamapori wanaokula Nyasi hivyo TAWA wanaendelea na mchakato wa kuleta wanyama wanaokula nyasi katika kisiwa hicho kwa upande wake Mwekezaji aliyeomba kuwekeza katika kisiwa hicho ameridhishwa na madhari ya kuvutia ndani ya kisiwa hicho hivyo anakusudia kujenga hoteli ya kitalii.
Fahamu maajabu ya mto Ruvuma ambao unaanzia milima ya Matogoro Manispaa ya Songea na kumwaga maji yake katika bahari ya Hindi.Mto huo una urefu wa takriban kilometa zaidi ya 800
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.