Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesikitishwa na kitendo kilichofanyika na wananchi wa Matemanga wilaya ya Tunduru kuharibu miundombinu ya maji ya bomba na kuacha maji yanapotea bure huku serikali ikitumia gharama kubwa kujenga miundombinu hiyo ambayo inatakiwa kulindwa na kutunzwa.
Mkuu wa Mkoa Ruvuma Christina Mndeme amekagua mradi wa maji wa Mkongogulioni wilaya ya Namtumbo ambao umetekelezwa na Serikali kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni mbili.Mradi unatarajia kuhudumia watu zaidi ya 8000.Wananchi hao hawajawahi kupata maji ya bomba tangu mwaka 1961.
Mkuu w Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amekagua na kuridhishwa na mradi wa maji ya bomba uliotekelezwa katika kitongoji cha Mingohi Kijiji cha Chimate wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma kwa shilingi milioni 50.
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.