Chama kikuu cha Ushirika cha wilaya za Mbinga na Nyasa MBIFACU kinatekeleza miradi mingi ambayo inaongeza mapato ya chama hicho na kuimarisha ushirika kwa wakulima mkoani Ruvuma.
Kampuni ya CHICCO inaendelea na kazi ya kukamilisha ujenzi wa uwanja wa ndege wa Songea ambapo serikali imetoa shilingi bilioni 39 kutekeleza mradi huo ambao mkataba wake unaishia Desemba 28,mwaka huu.Mradi umefikia asilimia 50 ambapo tayari ndege NDOGO zimeanza kutua kwenye uwanja mpya na ndege kubwa aina ya BOMBADIER zinatarajia kuruhusiw kuanzia Agosti mwaka huu.
Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Ruvuma imetembelea mradi wa Kituo cha afya Mkasale kata ya Namasakata wilaya ya Tunduru ambacho kimeanza kutoa huduma ya upasuaji baada ya serikali kutoa kiasi cha shilingi milioni 460 zilizokamilisha mradi huo na kuwaondolea kero wananchi ambao walikuwa wanasafiri umbali mrefu kutafuta huduma ambapo hadi sasa watu 51 wamefanikiwa kufanyiwa upasuaji na wote wapo salama
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.