Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajia kufungua jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Mji Mbinga na kukagua nyumba nane za Watumishi wa Halmashauri hiyo siku ya Januari 4 mwaka huu mjini Mbinga.
WAZIRI Mkuu Kasssim Majaliwa amesema sasa ni rasmi ndege ya kwanza ya abiria kupitia Kampuni ya ATCL inatarajia kutua katika kiwanja cha Ndege Songea Januari 15,2021.Waziri Mkuu ametoa ahadi hiyo kufuatia ombi la Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme alilolitoa wakati anatoa taarifa ya shughuli za maendeleo Mkoa wa Ruvuma katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi ya Waziri Mkuu Mkoani Ruvuma ambayo imeanza Janauri 2 hadi sita mwaka huu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameanza ziara ya kikazi katika Mkoa wa Ruvuma ambapo katika siku yake ya kwanza akiwa katika wilaya ya Tunduru ,mara baada ya kupokea taarifa ya shughuli za maendeleo Mkoa wa Ruvuma,pamoja na mambo mengine Waziri Mkuu alizungumzia mgogoro wa Kituo cha mabasi cha Tanga kilichopo Manispaa ya Songea ambapo ameagiza mgogoro huo umalizike haraka.
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.