Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amekataa kukabidhi madawati 50 na meza 10 katika shule ya msingi Mtakanini Halmashauri ya Namtumbo.Samani hizo zilizogharimu shilingi milioni 4 zimetengenezwa chini ya viwango.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ameviagiza vyombo vya sheria kutoa adhabu kali kwa wote wanaotumia dawa za kulevya aina ya bangi kwa kuwa wengi wanajihusisha kulima na kuvuta bangi mkoani Ruvuma.Alikuwa anazungumza kwenhye kilele cha wiki ya sheria nchini.
Kikao cha wadau wa maji mkoani Ruvuma kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma christina Mndeme kimepitisha azimio la kuwaondoa wote waliovamia vyanzo vya maji na kuendesha shughuli za kiuchumi ikiwemo Kilimo ili kulinda na kihifadhi vyanzo hivyo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadaye.
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.