Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 22 Aprili, 2020 amezungumza na Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama akiwa Chato Mkoani Geita kuhusu hali ya ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (Covid-19).Mhe. Rais Magufuli amewashukuru Watanzania kwa kuitikia wito wa kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona, na kwa kushiriki katika siku 3 za kumuomba Mwenyezi Mungu aepushe janga la ugonjwa huo.
Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma kimeunga kwa vitendo jitihada za serikali za kupambana na virusi hatari vya Corona baada ya kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni tatu.
WAtumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea wametekeleza maelekezo ya Rais Dkt John Magufuli kufanya maombi maalum ya kutokomeza virusi hatari vya Corona.Rais Ametoa siku tatu za kufanya ibada za maombi maalum ya kuliombea Taifa kuepukana na balaa la virusi vya corona
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.