Halmashauri zote nane mkoani Ruvuma zimepata hati safi kufuatia taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali katika mwaka unaoishia Juni 30 2021.Akizungumza katika kikao maalum cha CAG cha Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Madaba,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ameipongeza Halmashauri hiyo kuungana na Halmashauri nyingine za Mkoa wa Ruvuma kuweza kupata hati safi kufuatia ukaguzi wa CAG na kwamba Halmashauri ya madaba pia imefanya vizuri katika utoaji mikopo kwa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert ameipongeza Halmashauri ya Tunduru kwa kukusanya mapato kwa asilimia 106 ambapo Halmashauri hiyo katika kipindi 2020/2021 imeweza kukusanya zaidi ya shilingi bilioni tatu.Halmashauri hiyo pia imefanikiwa kupata Hati safi kufuatia ukaguzi wa CAGShow less
Ofisi ya Kamishna wa Aridhi Mkoani Ruvuma imezindua zoezi la upatikanaji Hati katika kata ya Ruhuwiko, Wilaya ya Songea.. Ambapo zeozi hilo llitamlahisishia mwananchi kupata Hat ndani ya siku moja bila kucheleweshewa kama mwanzo.
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.