Mkuu wa Mkoa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amekagua miradi inayotekelezwa kwa force akaunti Wilaya ya Namtumbo ambapo ameagiza ni lazima wananchi washirikishwe pia taratibu za fedha zifuatwe .
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ameziagiza Halmashauri zote nane kupitia wataalam wa afya kusimamia kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya wimbi la tatu la corona.RC Ibuge ametoa maagizo hayo wakati anazungumza na wakuu wa wilaya,wakurugenzi wa Halmashauri na watumishi wa umma ngazi ya Mkoa na wilaya zote kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Mwezeshaji Mwandamizi ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo cha Mipango na Maendeleo vijijini Dodoma Dkt Titus Mwageni ametaja maandalizi ya Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Halmashauri ya Madaba wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.