MKUU wa wilaya ya Songea amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali ( BALOZI) Wilbert Ibuge katika uzunduzi wa michezo ya umitashumta 2022 .
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma Kanali Thomas Laban amesikitishwa na tabia ya baadhi ya Wazazi na walezi kuwaficha watoto wenye ulemavu ndani hali inayosababisha kukosa haki yao ya msingi ya kupata elimu.Kanali Laban ameeleza masikitiko yake baada ya Watoto watatu tu wenye ulemavu wa viungo kupatikana katika Wilaya nzima yenye shule zaidi ya 100 kupokea msaada wa viti mwendo vilivyotolewa na serikali kwa lengo la kuwawezesha wenye ulemavu kuhudhuria masomo.Show less
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mheshimiwa Atupele Mwakibete amesema serikali imekamilisha kazi ya matengenezo ya meli katika Ziwa Nyasa hivyo Mkoa wa Ruvuma sasa unaweza kufikika kwa meli,ndege na barabara.Naibu Waziri Mwakibete alikuwa anazungumza na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ofisini kwake mjini Songea baada ya kumaliza ziara ya kikazi mkoani Ruvuma iliyolenga ukaguzi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha Ndege cha Songea ambapo serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 37 kutekeleza mradi huo.Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo amesema serikali imepata ahadi ya fedha kiasi cha Dola za Marekani milioni sita kutoka SADC kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi wa Reli ya kutoka Mtwara hadi Mbambabay.Amesema miradi hiyo ikikamilika ukiwemo mradi wa barabara ya Morogoro hadi Ruvuma na upanuzi wa barabara ya Songea hadi Njombe,Mkoa wa Ruvuma utakuwa moja ya Mikoa yenye miundombinu bora Tanzania.
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.