Rais Samia awezesha gari kufika kwa mara ya kwanza ,wananchi wasema malaika ameshukaSERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imewezesha kwa mara ya kwanza tangu uhuru gari kufika kwenye kijiji cha Ndonga Kata ya Riwundi Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.Serikali kupitia TARURA imetoa zaidi ya shilingi milioni 200 kutengeneza barabara ambayo haikuwepo tangu nchi kupata uhuru mwaka 1961.Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amekagua barabara hiyo ambapo amemshukuru Rais kwa kufungua Mawasiliano ya barabara katika kijiji hicho ambacho kiligeuka kisiwa.Serikali katika kijiji hicho licha ya kutengeneza barabara,pia imepeleka huduma ya umeme na kujenga zahanati.
Wananchi mkoani Ruvuma wameipongeza serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka ratiba ya safari za ndege za ATCL mara tatu kwa wiki.Abiria hao wametoa pongezi hizo wakati wanazungumza na Mwandishi wa habari hizi kwenye uwanja wa Ndege Songea.ATCL inatoa huduma za usafiri wa anga Kutoka Dar es salaam hadi Songea siku za Jumatatu,Jumatano na Ijumaa.Hata hivyo wananchi wameiomba serikali kuongeza safari kwa sababu hivi sasa abiria wanaotumia ndege za ATCL wameongezeka na ndege imekuwa inajaa.Meneja wa Uwanja wa Ndege Songea Jordan Mchami amekiri abiria ni wengi ambapo ndege yenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila inapofika na kuondoka inabeba abiria zaidi ya 70 na kwamba wanatarajia kuanza safari za usiku.
Mkoa wa Ruvuma umeingia mikataba 13 na wakandarasi yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni sita kwa ajili ya kutekeleza kazi mbalimbali za matengenezo ya barabara na ujenzi wa madaraja na makaravati.Mgeni rasmi katika hafla ya kuingia mikataba hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas.Meneja wa TARURA Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Wahabu Nyamzungu amesema mikataba hiyo ni utekelezaji wa hatua ya pili kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini TARURA Mkoa wa Ruvuma una mtandao wa kilometa 7146.22 ya mtandao mzima.
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.